Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sangoma mbaroni akidaiwa kubaka makaburini

Polisi 73781 Sangoma mbaroni akidaiwa kubaka makaburini

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara, linamshikilia mganga wa Kienyeji Sabihi Issa Mpando, mwenye umri wa miaka 41, mkazi wa Chipuputa manispaa ya Mtwara Mikindani akidaiwa kumbaka binti wa miaka 17, makaburini.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa alitumia mbinu ya kumlaghai kumpa matibabu binti huyo kwa masharti ya kumuingilia kimwili makaburini, huku akimweleza kuwa ni tiba.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Hamisi Ramadhani amethibisha kutokea kwa tukio na kufafanua kuwa limetokea Februari 23,2023 majira ya usiku katika eneo la makaburi ya Mingano.

Jeshi la Polisi limesema limebaini chanzo cha tukio hilo ni tamaa za mwili na kujistarehesha na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia leo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live