Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Salma atupwa jela miaka 34 kwa kutumia Twitter

Salma Jela Salma atupwa jela miaka 34 kwa kutumia Twitter

Thu, 18 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Salma Al-Shehab; ni mwanafunzi wa Saudi katika Chuo Kikuu cha Leeds, Uingereza ambaye alikuwa amerejea nyumbani kwao Saudia kwa likizo na kujikuta akihukumiwa kifungo cha miaka 34 jela kwa kuwa na akaunti ya Twitter.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardina la nchini Uingereza, Salma ni msomi mzuri na mwenye bidii ambaye alifika Uingereza mwaka 2018 au 2019 kusomea PhD yake katika Chuo Kikuu cha Leeds.

Salma alikuwa amerejea nyumbani, Saudi Arabia mnamo Desemba 2020 kwa likizo na alikuwa na nia ya kuwapeleka watoto wake wawili na mume wake nchini Uingereza. Lakini kabla ya kutekeleza azma yake hiyo, aliitwa kuhojiwa na mamlaka ya Saudi na hatimaye kukamatwa na kushtakiwa kwa Tweets zake.

Hukumu hiyo ya mahakama maalum ya kigaidi ya Saudia inatolewa wiki kadhaa baada ya ziara ya Rais wa Marekani, Joe Biden nchini Saudi Arabia ambayo wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wameonya kuwa inaweza kuutia moyo ufalme wa Saudia kuzidisha ukandamizaji wake dhidi ya wapinzani na wanaharakati wengine wanaounga mkono demokrasia.

Kesi hiyo pia ni mfano wa hivi punde zaidi wa jinsi mwanamfalme Mohammed bin Salman alivyowalenga watumiaji wa Twitter katika kampeni yake ya ukandamizaji, wakati huohuo akidhibiti hisa kubwa zisizo za moja kwa moja katika kampuni ya mitandao ya kijamii ya Marekani kupitia mfuko wa utajiri wa Saudia.

Kwa maelezo yote, Salma hakuwa mwanaharakati mkuu au hasa mwenye sauti kubwa Saudia, ama ndani ya ufalme au Uingereza.

Alijieleza kwenye Instagram ambapo alikuwa na wafuasi 159 -kama daktari wa meno, mwalimu wa matibabu, mwanafunzi wa PhD katika Chuo Kikuu cha Leeds na mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Princess Nourah bint Abdulrahman na kama mke na mama wa wanawe, Nuhu na Adam.

Wasifu wake kwenye Twitter walionesha alikuwa na wafuasi 2,597. Miongoni mwa tweets kuhusu uchovu wa COVID na picha za watoto wake wadogo wakati mwingine ali-retweet tweets za wapinzani wa Saudi wanaoishi uhamishoni ambao walitaka kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa katika ufalme huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live