Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sabaya na wenzake wafikishwa Mahakamani kusikiliza hukumu yao

Sabayaaa.jpeg Sabaya na wenzake wafikishwa Mahakamani kusikiliza hukumu yao

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

liyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ambayo leo Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Mbali na Sabaya watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Leo Jumanne Mei 31, 2022 Sabaya na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo saa 3:09 asubuhi

Hukumu ya leo inatarajiwa kuamua hatma ya kiongozi huyo wa zamani na wenzake endapo wataachiwa huru, kwani hadi sasa mbali na kesi hii hawana kesi nyingine.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27/2021, Jamhuri ilikuwa na mashahidi 13 huku utetezi wakiwa na mashahidi nane ambapo watuhumiwa hao walikuwa wakitetewa na jopo la mawakili watano huku Mwahomange akijitetea mwenyewe.

Machi 31 mwaka huu Hakimu Patricia Kisinda, alisema atatoa hukumu hiyo leo baada ya pande zote kuwasilisha hoja zao za majumuisho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: