Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sabaya kutinga tena mahakamani leo

Sabaya Mko.jpeg Sabaya kutinga tena mahakamani leo

Mon, 18 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake, inatarajiwa kutajwa tena leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kesi hiyo iliahirishwa Julai 4 mwaka huu baada ya upande wa Jamhuri kuieleza mahakama kwamba upelelezi wa shauri hilo ulikuwa haujakamilika.

Upande wa utetezi katika kesi hiyo ulitaka upande wa Jamhuri umalize upepelezi wake ili kesi hiyo ianze kusikilizwa na ukadai kuwa wateja wao walikuwa wanateseka.

Mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya hakimu mkazi Moshi, Salome Mshasha, wakili wa utetezi, Helena Mahuna aliuomba upande wa Jamhuri uharakishe upatikanaji wa kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) cja kuruhusu kusikilizwa kesi hiyo.

Awali upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili Serikali Mwandamizi, Kasimu Daudi aliyeambatana na wakili mwenziye, Sabikia Mcharo uliieleza mahakama kwamba upelezi ulikuwa haujakamilika na walikuwa hawajapata kibali cha kusikiliza kesi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live