Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sabaya kuhukumiwa October 1, 2021

Hatima Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai

Tue, 24 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imehitimisha usikilizwaji wa kesi ya jinai namba 105 ya mwaka 2021, inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo amesema hukumu ya kesi hiyo ni Oktoba, 2021.

Hakimu huyo ametoa siku saba kwa pande zote kuwasilisha mawasilisho ya maandishi kuhusu kesi hiyo. hoja hiyo ya mawasilisho iliwasilishwa na wakili wa Serikali Tumaini Kweka akitaka waongezewe muda kwa siku hizo saba.

Kesi hiyo imetumia zaidi ya siku 30 tangu kuanza kusikilizwa, Sabaya na wenzake wanashitakiwa kwa kesi ya unyanganyi kwa kutumia silaha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live