Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sabaya kortini tena leo

SABAYA PEKE YAKE Sabaya kortini tena leo

Mon, 26 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi leo Septemba 26, 2022 itaendelea kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi namba 2, 2022, dhidi ya Lengai Ole Sabaya, kinatarajiwa kupata jibu leo.

Sabaya aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, leo atapandishwa katika mahakama hiyo akiwa peke yake baada ya wenzake kuachiwa huru Septemba 6 mwaka huu.

Mshitakiwa huyo pia anatarajiwa kubadilishiwa hati ya mashitaka ili kumtaja peke yake tofauti na ilivyokuwa awali. Washitakiwa wenzake wanne walikiri makosa na wakatozwa faini na kuachiwa huru na mahakama hiyo iliyoongozwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi, Salome Mshasha.

Washitakiwa hao Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey waliingia makubaliano na ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP), wakasomewa mashitaka mengine mawili ambayo walitiwa hatiani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live