Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sabaya augua mahabusu

OLE SABAYA HAI Lengai Ole Sabaya

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Kesi inayomkabili aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Jumatano Agosti 4, 2021 imeahirishwa hadi kesho kwa kuwa Sabaya ni mgonjwa.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana Jumanne shauri la Sabaya lilipangwa kuendelea kusikilizwa leo ambapo shahidi wa saba wa jamhuri ambaye ni mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Wilaya ya Arusha, ASP Gwakisa Minga alikuwa aendelee na ushahidi wake.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo, mkaguzi msaidizi wa Magereza, Ramadhani Misanga ameieleza mahakama kuwa alipata taarifa kutoka kwa Mkuu wa gereza kuu ya Arusha kuwa mshtakiwa wa kwanza (Sabaya) anaumwa hivyo hatoweza kufika mahakamani.

Hakimu Amworo amekubaliana na maombi hayo na kuahirisha kesi hadi kesho.

Chanzo: Mwananchi