Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sabaya augua, kesi yahairishwa

Sabaya Kesi Pic Sabaya augua, kesi yahairishwa

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita leo Jumatano Novemba 3, 2021 imeahirishwa hadi kesho kwa kuwa Sabaya ni mgonjwa.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana shauri la Sabaya lilipanga kuendelea kusikilizwa leo ambapo shahidi wa upande wa Jamhuri ambaye ni Ofisa wa Tehama wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Jofrey Nnko, alikuwa aendelee kutoa ushahidi.

Wakili wa utetezi Mosses Mahuna aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi kesho Alhamisi Novemba 4, 2021 kuwa Sabaya ni mgonjwa na wamepokea taarifa hizo leo asubuhi.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Patricia Kisinda amekubali maombi hayo na kuahirisha kesi hiyo hadi kesho Novemba 4.

Chanzo: mwananchidigital