Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sabaya aomba kuhamishwa Mahakama

Sabaya Pic Sabaya aomba kuhamishwa Mahakama

Tue, 30 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Upande wa utetezi katikaa kesi ya uhujumu uchumi namba 2 ya mwaka 2022, inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, na wenzake wanne wameomba shauri hilo kuhamia Mahakama Kuu ili kesi hiyo ianze kusikilizwa na washtakiwa wajue hatma yao.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, wakili wa utetezi, Hellen Mahuna, ameiomba mahakama kulihamisha shauri hilo mahakama ya juu kwani mahakama ya sasa haina uwezo wa kuisikiliza kesi hiyo.

Amesema kuhamishwa kwa maelezo, vielelezo, ushahidi na masuala mengine kutaipa Mahakama Kuu uwezo wa kuendeleza shauri hilo ikiwa ni baada ya kuchukua muda mrefu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi ambayo haijapata kibali cha kusilikiza kesi hiyo.

Wakili Hellen ameieleza mahakama hiyo kwamba washtakiwa katika kesi hiyo, hususani mshtakiwa wa kwanza Ole Sabaya ambaye anaumwa, wanaendelea kuteseka gerezani bila kujua hatma yao jambo ambalo halileti picha nzuri.

Akitupilia mbali,hoja za utetezi iliyotolewa Agosti 12, 2022 kutaka Mahakama itazame kifungu cha 62 cha tafsiri ya sheria kuwa endepo sheria haijatoa ukomo wa jambo kufanyika, jambo hilo lifanyike kwa uzoefu, Hakimu Mshasha amesema hoja hiyo haina msingi.

Amesema kifungu hicho hakiwezi kutumika katika kesi ya uhujumu uchumi lakini pia mahakama haina mamlaka ya kumuamuru DPP kutoa kibali cha kusikiliza kesi hiyo bali jambo hilo litafanyika baada ya ofisi hiyo kujiridhisha na kile inachopanga.

Akijibu hoja za utetezi, wakili wa serikali, Sabitina Mcharo, amesema wamesikia hoja hizo pamoja na rai ya mahakama na kwamba watafanyia kazi jambo hilo ili upelelezi ukamilike na kesi ianze kusikilizwa.

Hakimu Mshasha ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 12, 2022 itakapotajwa tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live