Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sabaya alimpora milioni 90 Mroso na kwenda 'kula bata'

5 Sabaya alimpora milioni 90 Mroso na kwenda 'kula bata'

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: ippmedia.com

Ofisa Uchunguzi wa TAKUKURU,Ramadhani Juma(39) ambaye ni Shahidi wa 13 katika kesi ya uhujumu namba 27, inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya,ameelezea mchanganuo wa mgawanyo wa fedha Sh.milioni 90 zinazodaiwa kuchukuliwa kwa mfanyabiashara Francis Mroso.

Shahidi huyo amedai Sabaya, alikabidhiwa fedha kiasi cha Sh.milioni 90 na kijana wake, akiwa kati eneo la AIM MALL Mtaa wa Majengo jijini Arusha.

Amedai kwamba fedha hizo, alipewa kwa kumlazimisha mfanyabiashara Francis Mroso,na alipokabidhiwa aliziingiza katika gari la Serikali STL 5434, na baada ya hapo, walikwenda kula maisha na vijana wake katika Hoteli ya Tulia Lodge iliyopo Sakina mkoani humo.

Baada ya kazi mgao ulikuwa hivi John Odemba Sh.300,000, Sadick Kiiza 400,000, Nathan Msuya Sh.Sh.500,000, Watson Sh.600,000, Enock Togolani Sh.milioni 1.5, Silvester Nyegu Sh.milioni 2.2 na Jakson Macha Sh.milioni 1.4. 

Chanzo: ippmedia.com
Related Articles: