Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sabaya akiri kumiliki silaha "Naitumia Kujilinda"

Sabaya 2?fit=680%2C453&ssl=1 Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya HAI, Ole Sabaya

Thu, 19 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha ameieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa anamiliki silaha aina ya Glock-17 kwa ajili ya kujilinda kutokana na kutishiwa kuuawa.

Akihojiwa na wakili wa Serikali mkuu, Tumaini Kweka leo Alhamisi Agosti 19, 2021 mbele ya hakimu mkazi mwandamizi, Odira Amworo, Sabaya amesema silaha hiyo alianza kuimiliki Machi 24, 2021.

Sehemu ya mahojiano hayo alikuwa hivi;

Wakili: Tusaidie katika ushahidi wako wa msingi umeieleza mahakama unamiliki silaha

Sabaya: ni sahihi

Wakili: Unamiliki silaha ya aina gani

Sabaya: Hakimu kwa sababu ni kifaa cha moto sijui kitatumikaje nikieleza kilivyo.

Wakili: Nataka kujua ni silaha

Sabaya: Kwa usalama wa silaha hiyo na kwa sababu nipo gerezani naomba nisieleze silaha gani. Ni silaha ndogo inaitwa Glock 17

Wakili:Utakubaliana na mimi kwa Kiswahili inaitwa bastola

Sabaya: Hapana

Wakili: Ulikua unaimiliki kwa shughuli gani

Sabaya: matumizi ya ulinzi binafsi

Wakili: Unapokuwa wapi

Sabaya: Ninapokuwa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro

Wakili: Hai ulikuwa una maadui

Sabaya: Ndiyo mheshimiwa hakimu

Wakili: Ulianza kumiliki lini?

Sabaya: Nilianza kuimiliki Machi 24, 2021

Soma zaidi:Ole Sabaya asomewa maelezo upya, akana

Wakili: Kwenye ushahidi wako wa msingi siku ukiondoka kuja Arusha Februari 9, 2021 uliacha silaha yako nyumbani Bomang'ombe.Ni sahihi siku ile ulikuwa ukimiliki silaha?

Sabaya: Sikuwahi kumiliki silaha ya moto kwa wakati huo nilikuwa na silaha ila haikuwa silaha ya moto

Wakili: Una watoto wangapi

Sabaya:Kwa sababu nimeshasema familia iko kwenye risk. Naomba nisitaje watoto wala idadi

Wakili: Lengai nikurudishe kwenye swali dogo wakati unatoka Hai saa 9 kuja Arusha na hiyo timu yako ulipita wapi?

Sabaya: Nilipitia Kia barabara ya Mirerani nikaja Arusha

Wakili: Kwanini ulipita huko usipite barabara ya kawaida Moshi -Arusha

Sabaya: Napitia barabara yoyote kwa usalama wangu kwa sababu natishiwa kuuawa

Wakili: Kwanini ulikuwa unatishiwa kuuawa na wewe ni kiongozi wa watu

Soma zaidi:Sabaya amkana mshirika wake katika kesi

Sabaya: Kwa sababu ya aina ya majukumu niliyokuwa nafanya siasa za Arusha na Hai

Wakili: Umefika Arusha mlipokuwa mnaenea na timu yako alimkuta shahidi wa nne Hajirin Saad Hajirin, ulimuona?

Sabaya: Ndio nilimuoma hapa mahakamani

Wakili: Wewe unafahamaniana naye

Sabaya: Hapana

Wakili: Una ugomvi naye

Sabaya: Kama simfahamu siyo rafiki wala adui

Wakili: Na yule shahidi wa pili kutoa ushahidi wake akasema alikuona Shahidi Store (dukani) una ugomvi naye au unamfahamu?

Sabaya: Simfahamu na hapo Shahidi Store sipafahamu

Sabaya na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura wanashtakiwa kwa makosa matatu ya unyang'anyi wa kutumia silaha katika duka la Mohamed Saad eneo la bondeni jijini Arusha Februari 9, 2021.

Chanzo: Mwananchi