Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sabaya afikishwa Mahakama Hakimu Mkazi Moshi leo

SABAYA PEKE YAKE Sabaya afikishwa Mahakama Hakimu Mkazi Moshi leo

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amefikishwa kwa mara nyingine tena leo April 5, 2023 katika Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi.

Juni Mosi, 2022 Sabaya na wenzake wanne walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi wakikabiliwa na mashtaka 7 ikiwemo uhujumu uchumi.

Septemba 6 mahakama hiyo iliwaachia huru washtakiwa wanne, Sylivester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey baada ya kukiri kutenda makosa ambapo mahakama iliwatia hatiani na kuwaamuru kulipa kila mmoja faini ya Sh50,000 na fidia ya Sh1 milioni kwa waathirika wa tukio hilo ambaye ni Alex Swai.

Hata hivyo, Machi 29, mwaka huu alipofikishwa mahakamani hapo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Sabitina Mcharo aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo namba mbili ya mwaka 2022 umekamilika na kuiomba mahakama hiyo kuwapa tarehe ya karibu kwa ajili ya kuweka vibali pamoja na kuendelea na taratibu nyingine kwa mujibu wa sheria.

Chanzo: mwanachidigital