Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sabaya aendelea kusota Gerezani, Kesi yapigwa kalenda

SABAYA PEKE YAKE Sabaya aendelea kusota Gerezani, Kesi yapigwa kalenda

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Ole Sabaya ataendelea kusota mahabusu katika gereza la Karanga mjini Moshi hadi Desemba 12, 2022 kutokana na kesi yake kuahirishwa, baada ya hakimu aliyetakiwa kuisikiliza kuwa katika majukumu mengine.

Kesi hiyo ilikuwa itajwe leo Desemba 5, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Salome Mshasha, lakini wakili wa Serikali, Susan Kimaro akaeleza hakimu yuko kwenye majukumu mengine.

Sabaya na wenzake wanne ambao wao baadaye waliachiwa huru baada ya kukiri makosa yao kwa kukubaliana na DPP, walifikishwa kortini kwa mara ya kwanza Juni Mosi, 2022, wakikabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi ikiwamo utakatishaji fedha.

Mshitakiwa huyo alikanusha mashitaka hayo na upande wa Jamhuri ulishaieleza mahakama kuwa upelelezi ulishakamilika na wako tayari kuwasilisha vibali hivyo vya DPP isipokuwa kumekuwa kukitokea udhuru kwa upande wa hakimu.

Kesi hiyo imeahirishwa Desemba 12 mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live