Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sabaya abaki gerezani, wenzake waachiwa huru

Sabaya Hukumuni Ole Sabaya

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watuhumiwa wanne katika kesi namba mbili ya mwaka 2022 ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekua mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, wameachiliwa huru, baada ya kuandika barua ofisi ya DPP ya kuomba wakae meza ya makubaliano ili walipe faini na fidia.

Watuhumiwa waliochiliwa huru ni Sylivester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Asey huku mtuhumiwa namba moja katika kesi hiyo Lengai Ole Sabaya akibaki magereza kuendelea na shauri hilo.

Mkurugenzi Msaidizi wa kutenganisha upelelezi na mashtaka Marternus Marandu, amesema mnamo Agosti 3, 2022, washtakiwa hao wanne waliandika barua katika ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa serikali kuomba kukaaa meza ya makubaliano ili kuweza kulipa faini na fidia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live