Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu ya kukamatwa ‘Nabii Tito’ hii hapa, Kamanda wa Polisi Dodoma amefunguka

1788 RPC DODOMA 660x400

Tue, 23 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Leo January 23, 2018 Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma limethibitisha kumkamata Tito Onesmo Machibya ambaye anajiita ‘Nabii Tito’ ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nong’ona kilicho nyuma ya Chuo Kikuu cha Dodoma.

Kamanda wa Polisi Dodoma Gilles Muroto ameeleza kuwa January 16, 2018 mtuhumiwa huyo alikamatwa na Jeshi hilo la Polisi akituhumiwa kurusha vipande vya matangazo ya video na picha vyenye maudhui ya kukashfu dini nyingine na kuleta chuki dhidi ya watu wengine.

“Kijana huyu ameonekana akirusha kwenye mitandao ya kijamii na kusambaza vipeperushi  kwenye maeneo ya starehe, kutangaza dini inayokiuka maadili ya nchi hadharani na kufanya vitendo ambavyo havifai na kutumia kitabu cha Biblia ambacho hafungamani nacho.” – Kamanda Mroto

LIVE: Jeshi la Polisi Kinondoni wazungumza kuelekea uchaguzi mdogo Feb 17



 

Chanzo: millardayo.com