Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu ushahidi kesi ya Shamim, mumewe kukwama kuendelea

MADAWAA.webp Sababu ushahidi kesi ya Shamim, mumewe kukwama kuendelea

Fri, 29 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa maarufu kama Mafisadi imeshindwa kuendelea kusikiliza ushahidi baada ya upande wa Jamhuri katika kesi hiyo kudai kuwa shahidi wao ni mgonjwa.

Kesi hiyo namba 4/2020 inawakabili Abdul Nsembo (45) na mke wake Shamimu Mwasha (41), imepangwa kuendelea leo mahakamani hapo.

Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Elinaza Luvanda, imeagiza mawakili wa pande zote mbili kuwasiliana kabla ya kufika mahakamani ili kupunguza usumbufu wa kusitisha kazi nyingine wakati kesi haiwezi kuendelea kusikilizwa.

Awali, Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, alidai kuwa shahidi waliyekuwa wanamtegemea ameshindwa kufika mahakamani kwa sababu ni mgonjwa, hivyo aliomba kesi hiyo kuendelea leo.

Wakili wa utetezi, Nassoro Juma, alidai kuwa ili kesi iweze kuendelea kama ilivyopangwa, Jamhuri waite mashahidi zaidi ya mmoja ikitokea mwingine ana dharura kesi iweze kusikilizwa.

Jaji alisema ili kuepusha usumbufu, mawakili pande zote mbili wawasiliane na Msajili ili kuondoa usumbufu pale anapokosekana shahidi.

Alisema kesi hiyo itaendelea leo kusikilizwa ushahidi wa Jamhuri.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanadaiwa kusafirisha dawa hizo za kulevya, Mei mosi, mwaka jana wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live