Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu kesi ya Zitto Kabwe kupigwa kalenda

78805 Pic+zitto

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe baada ya kuelezwa kuwa mshtakiwa huyo ambaye ni kiongozi wa chama hicho amefiwa.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga amedai mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Huruma Shaidi kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Soma zaidi: Shahidi kesi ya Zitto aeleza alivyowapokea majeruhi wanaodaiwa kumuua polisi

Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala amedai leo Jumatatu Oktoba 7, 2019 kuwa mteja wake amefiwa mkoani Kigoma, anaomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Shaidi ameahirisha shauri hilo hadi Oktoba 22 na 23, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Soma zaidi: Shahidi kesi ya Zitto aeleza jinsi askari polisi, wananchi walivyouawa

Pia Soma

Advertisement
Tayari mashahidi wanne wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi katika kesi hiyo akiwemo Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, John Makungu.

Katika kesi ya msingi, Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi anayodaiwa kuyatenda  Oktoba 28, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama hicho.

Soma zaidi: Shahidi aliye masomoni akwamisha kesi ya Zitto

Chanzo: mwananchi.co.tz