Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu kesi ya Sabaya kukwama hizi hapa….

7264e9cfae641babfa8b07e9d5d66ddc.jpeg Sababu kesi ya Sabaya kukwama hizi hapa….

Thu, 10 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya Uhujumu Uchumi,Utakatishaji fedha haramu na kumiliki Genga la Uhalifu inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (35) na wenzake sita imehairishwa hadi march 14 mwaka huu.

Kesi hiyo iliyokuwa inaendelea leo Machi 10, 2022 imehairishwa baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Patricia Kisinda kuwa na majukumu mengine ya kiofisi nje ya Jiji la Arusha.

Akiharishwa kesi hiyo, Hakimu Mkazi,Pamela Meela aliwataka mawakili wa upande wa utetezi na waendesha mashitaka wa serikali kujipanga siku hiyo ya Machi 14 mwaka ili kesi hiyo iweze kuendelea kwa kuwa Hakimu Kisinda atakuwa amerudi.

Kabla ya kuhairishwa juzi mchana, wakili Edmund Ngemela alikuwa akiendelea kumwongoza shahidi wake wa tano Jackson Macha {30} mbele ya Hakimu Kisinda na kudai kuwa hajawahi kupokea mgao wa Sh milioni 1.4 kutoka kwa Sabaya kufuatia rushwa ya Sh milioni 90 aliyodaiwa kupewa.

Alidai mgao wa Sh milioni 1.4 uliokuwa ukitolewa na Sabaya katika Lodge ya Tulia ya Jijini Arusha hahusiki nao kwani hajawahi kuomba wala kushawishi rushwa ya kiasi hicho wala kupokea mgao huo.

Mbali ya Sabaya washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na Enock Mnkeni (41),Watson Mwahomange (27) maarufu kwa jina la Malingumu, John Aweyo (45),Syliverster Nyegu (26) maarufu kwa jina la Kicheche ambaye pia ni msaidizi wa Sabaya, Jackson Macha (29) na Nathan Msuya (31).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live