Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu CHADEMA kuzuiwa kumuona Mbowe

Sababu Kuzuia Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Baadhi ya makada wa CHADEMA waliofika kumuona Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe juzi katika gereza Ukonga jijini Dar es Salaam, hawakutimiza lengo lao baada ya askari Magereza waliokuwa getini kuwazuia wakisema kuwa wamepata maelekezo kutoka juu.

Hata hivyo, Msemaji wa Magereza Kamishna Msaidizi, Justin Kaziulaya alipoulizwa kwa simu jana alikiri kuwazuia akisema ni kutokana na idadi yao kuwa kubwa jambo alilosema linaakiuka masharti ya kupambana na maambukizo ya Uviko-19.

“Ukiangalia kwa haraka haraka picha za watu walioenda kumuona Mbowe jana, Mkuu wa Gereza alikuwa anatekeleza maagizo ambayo yanafuatwa kwa magereza yote nchini na sio kwa mhalifu fulani,” alisema.

Mbowe alikamatwa Julai 30 jijini Mwanza na kuunganishwa na wenzake watatu katika kesi inayohusisha kupanga njama za kufanya ugaidi inayoendelea kusikilizwa na Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia taarifa hizo kwa simu, Mkurugenzi wa Uhusiano, Itifaki na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema hatua ya kuwazuia kumwona Mwenyekiti wao inazua hofu kuhusu hali yake.

“Walisema kuwa wanaoruhusiwa ni wenye vibali tu, jambo ambalo sio sahihi kwani siku za mwisho mwa juma na sikukuu ni siku ya kutembelea wafungwa na mahabusu.

“Wenye vibali wanaweza kwenda siku yoyote kama ambavyo Mawakili wanaweza kwenda Gerezani siku yoyote,” alisema.

Mrema aliwataja waliozuiwa ni John Heche, Julius Mwita na wagombea Ubunge wa mwaka 2020 kutoka majimbo mbalimbali nchini na wanachama wengine wa Mkoa wa Dar es Salaam na hata walipoomba kumuona Mkuu wa gereza hawakufanikiwa kwa hoja kwamba yuko kwenye kikao.

Alisema iliwafanya kukaa pale mpaka mchana na kulazimika kuondoka bila kumuona.

Chanzo: mwananchidigital