Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saba mbaroni wakituhumiwa kwa mauaji Mwanza

Mbaroniiiiiiiii Saba mbaroni wakituhumiwa kwa mauaji Mwanza

Wed, 24 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kinawashikilia watu saba kwa mahojiano kuhusu mauaji ya wanawake wawili wakazi wa Wilaya ya Magu yaliyotokea katika matukio tofauti.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mei 23, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema matukio hayo ya mauaji yanayohusishwa na imani za kishirikina yametokea kati ya April 26, 2023 na Mei 10, 2023.

Katika tukio la kwanza, Kamanda Mutafungwa amesema jeshi hilo linawashikilia Masunga Mabula (32), Salome Raphael (32) na Ezekiel Charles (54) ambaye ni mganga wa kienyeji, wote wakazi wa Wilaya ya Magu wakituhumiwa kwa tuhumza ma mauaji ya Ester Lukonu (51), mkazi wa kijiji cha Bughamangala wilayani Magu.

“Mei 10, 2023, Jeshi la Polisi lilipokea taarifa ya mauji ya Ester Lukonu (51) ambaye katika uchunguzi wa awali alibainika kuuawa kwa kukabwa shingoni na mwili wake kutelekezwa kwenye shamba la mihogo,’’ amesema Kamanda Mutafungwa

Amesema uchunguzi huo pia ulibaini uwepo wa mipira ya kiume katika eneo la tukio, hali inayoonyesha kuwa wauaji pia walimwingilia marehemu kimwili kabla ya kumuua.

Kamanda Mutafungwa amesema uchunguzi wa kitabibu umebaini kuwa marehemu Ester alikatwa sehemu za siri, hali inayoonyesha mauaji hayo yanahusiana na imani za kishirikina.

“Jeshi la Polisi limefanikiwa kumtia mbaroni mganga wa kienyeji aliyepokea sehemu za siri za marehemu kama sharti la kuwaagua wateja wake,’’ amesema Kamanda huyo wa polisi

Katika lingine, Kamanda Mutafungwa amesema jeshi hilo linawashikilia watu wanne kwa mahojiano kuhusu mauaji ya Katalina Ruzari, mkazi wa kijiji cha Matale Wilaya ya Magu lililotokea April 26, mwaka huu.

Amewataja wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kumuua Katarina kwa kumkata shinga na kitu chenye ncha kali kuwa ni Yunis Runzali (50), Bernadi William (86), Maguta Chandaruba (48) na Mashaka Maduka (43) wote wakazi wa Kijiji cha Matale wilayani Magu.

Mauaji hayo yanadaiwa kuchochewa na imani za kishirikina baada ya kuwepo madai kuwa wakati wa uhai wake, marehemu alijihusisha na masuala ya kishirikina

Chanzo: www.tanzaniaweb.live