Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saba mahakamani kwa uhujumu uchumi Dar

Saba Mahakamani Kwa Uhujumu Uchumi Dar Saba mahakamani kwa uhujumu uchumi Dar

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: millard

Wakazi saba wa Jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mbele ya mahakimu watatu tofauti wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka manne yakiwamo ya kusafirisha sukari na mafuta ya kupikia kwa magendo vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 10.7.

Mashtaka mengine ni kukwepa ushuru chini ya kifungu 148(e) cha sheria ya forodha, kusafirisha mizigo ya magendo kushindwa kuwasilisha nyaraka za bidhaa za magendo na kukutwa na bidhaa za magendo

Washitakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Veneranda Kaseko, Mahakimu Wakazi, Nabwike Mbaba na Ramadhani Rugemalira.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali Anderson Lukosi akisaidiana na wakili kutoka TRA, Auni Chilamula amewataja washtakiwa hao kuwa ni Mfanyabiashara Mustapha Bakari (30) Mkazi wa Kunduchi, mafundi Mohamed Nassor(25) na Abdulmajid Kheri (17) na dereva Erick Solomon Mwagemba (25).

Wengine ni dereva Justin Mollel (35) pamoja na Wavuvi Mbaraka Mwanjovu (23) na Hamad Hamad maarufu Katoto (23).

Mbele ya Hakimu Nabwike Mbaba, washtakiwa Nassoro na Kheri wanadaiwa Februari 11, mwaka huu maeneo ya Kunduchi wilayani Kinondoni Dar es Salaam, walikutwa wakiingiza mifuko 20 ya sukari kwa kutumia njia ya magendo bila ya kulipa kodi na kukwepa ushuru wa Sh. 2,335,697.93 kinyume na sheria.

Chanzo: millard