Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rushwa ya ngono yamweka matatani mtumishi Tanesco

66142 Pic+ngono

Wed, 10 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) mkoani Mtwara inamshikilia ofisa utumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Jumanne Songoro kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mlalamikaji ambaye jina lake limehifadhiwa ili kumpangia majukumu mapya ya kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Julai 9, 2019, kamanda wa Takukuru  wa Mtwara, Stephen Mafipa amesema aliomba rushwa hiyo ili aweze kumpangia mlalamikaji majukumu mengine katika kitengo cha kudumu kulingana na kiwango chake cha elimu baada ya kubadilishiwa majukumu ya awali kufuatia maagizo kutoka Tanesco makao makuu.

Kamanda Mafipa amesema jana majira ya saa nane mchana walimkamata mtuhumiwa huyo kwani ni kinyume na kifungu cha 25 cha sheria ya kuzuia na kupamba na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 na kwamba atafikishwa mahakamani.

“Uchunguzi umebaini mtuhumiwa alianza kushawishi rushwa ya ngono kutoka kwa mlalamikaji kwa nyakati tofauti toka Disemba 2018 na ndipo Julai 4, 2019 mlalamikaji aliwasilisha malalamiko katika ofisi ya Takukuru mkoa tukafanya uchunguzi na baada ya kujiridhisha kuna mazingira ya rushwa tuliweka mtego na kufanikiwa kumkamata,” amesema Mafipa

Amesema mtuhumiwa alikamatwa akiwa na mlalamikaji katika mojawapo ya vyumba vya nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Mtwara Mikindani akia tayari kutekeleza adhima ya kupokea rushwa ya ngono.

Chanzo: mwananchi.co.tz