Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Rushwa ya ngono ina inatudidimiza’

Sat, 12 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Licha ya juhudi za kuwawezesha na kuwajengea uwezo wa kushindana katika soko makandarasi wa kike nchini, rushwa ya ngono inadaiwa kuwa miongoni mwa changamoto na vikwazo kwa makandarasi hao kupata kazi.

Hali hiyo inatokana na kudaiwa rushwa ya ngono kama masharti ya kupata kazi na wanapo kataa kujikuta wakikosa kazi hata baada ya kufanikiwa kupenya katika mchakato wa zabuni.

Hayo yalielezwa jana jijini Mwanza na mmoja wa makandarasi wa kike, Bahati Christopher kwenye mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo makandarasi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

“Bodi ya wakandarasi lazima iingilie kati kuchunguza kwa kushirikiana na vyombo husika kushughulikia changamoto hii ya wakandarasi wa kike kuombwa rushwa ya ngono hata pale wanapotimiza masharti na vigezo vyote.”

“Wakati mazungumzo kwa wakandarasi wa kiume huishia ofisini, hali ni tofauti kwa sisi wa kike kwani mwisho wa mazungumzo utapewa ‘business card’ na maelekezo ya kukutana hotelini kukamilisha mazungumzo,” alisema.

Akizungumzia madai hayo, mwenyekiti wa bodi ya usajili wa wakandarasi (CRB), Consolata Ngwimbwa aliwataka makandarasi wa kike kujiamini kitaaluma na kulinda hadhi, utu na heshima yao kwa kusema hapana pale mazungumzo ya kikazi yanapohamia kwenye ngono.

“Mtu anapoacha kuzungumza masuala ya kazi na kuhamia kwenye ngono toa taarifa kwa mamlaka husika ikiwamo Takukuru). Wanawake tusiwe wanyonge kwa sababu unyonge wetu wakati mwingine ndiyo unakaribisha mambo haya,” alisema Ngwimbwa.

Akizungumzia ushindani dhidi ya wakandarasi wa nje wenye uwezo kimtaji na utaalam, aliwataka makandarasi nchini kuungana kuomba kazi kwa pamoja badala ya kila mmoja kuomba kivyake.



Chanzo: mwananchi.co.tz