Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rushwa ya Sh200,000 yampeleka jela miaka mitatu

12464 PIC+MAHAKAMANI TanzaniaWeb

Fri, 17 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Mahakama ya Wilaya ya Same, imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela, katibu wa Baraza la Ardhi la Kata ya Myamba, Kiondo Angalo, baada ya kumtia hatiani kwa makosa mawili ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh200,000.

Hukumu hiyo imetolewa leo  Agosti 17,2018 na Hakimu wa Ferdinand Kigingi, ambaye  alimhukumu kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh500,000 kwa makosa hayo.

Hakimu amesema mahakama hiyo imeridhishwa na ushahidi wa upande wa mashitaka ulioongozwa na wanasheria wawili wa Takukuru, Rehema Mteta na Caroline Lugenge.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Takukuru Mkoa Kilimanjaro, Holle Makungu imesema kuwa katika hukumu hiyo, mahakama  iliridhika na ushahidi huo kuwa Katibu huyo alipokea fedha hizo kutoka kwa Mhina Mbasha.

Katika shitaka la kwanza, waendesha mashtaka hao wa Takukuru walidai kuwa, mwaka 2017, mshtakiwa alishawishi apewe rushwa ya Sh200,000 ili aweze kumpatia Mbasha nakala ya hukumi ambayo ingemsaidia kukata rufaa.

Mbasha alikuwa ameshindwa katika shauri la ardhi namba 2/2017 hivyo alikuwa ameomba fedha hizo ili aweze kumpatia nakala ya hukumu ili aweze kukata rufaa katika baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Same.

Katika shitaka la pili, katibu huyo anadaiwa kupokea kiasi hicho cha fedha ili aweze kutoa nakala hiyo ya hukumu pamoja na nakala ya mwenendo wa shauri hilo a ardhi.

Kwa mujibu wa Makungi, katibu huyo amepelekwa gerezani kuanza kutumikia kifungo hicho cha miaka mitatu jela, baada ya kushindwa kulipa faini hiyo ya Sh500,000.

Chanzo: mwananchi.co.tz