Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rugemalira na wenzake kuendelea kusota gerezani

Lugemarira2 Rugemalira na wenzake kuendelea kusota rumande

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: mwananchidigital

Upelelezi wa kesi ya Uhujumu uchumi namba 27/ 2017, inayomkabili Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), James Rugemalira na mwenzake haujakamilika.

Rugemalira na aliyekuwa Mwanasheria wa IPTL, Joseph Makandege wanaokabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya kutakatisha fedha.Wakili wa Serikali Faraja Ngukah ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Septemba 9, 2021 wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa, kuwa upelelezi bado haujakamilika wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya kutajwa, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

"Kesi hii imeitwa leo kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri hili bado haujakamilika, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili kutajwa," amesema Ngukah.

Ngukah baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 23, 2021 itakapotajwa.

Hata hivyo leo, washtakiwa hao wahakuletwa mahakamani hapo kusikiliza shauri lao.

Chanzo: mwananchidigital