Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rufaa ya Mbowe, Matiko yakwama

29259 Pic+mbowe+kwama TanzaniaWeb

Thu, 29 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rufaa ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Esther Matiko kupinga kufutiwa dhamana leo imekwama kusikilizwa.

Rufaa hiyo imekwama kusikilizwa kutokana na kukosekana kwa mwenendo na uamuzi wa kuwafutia dhamana, hivyo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupanga kusikilizwa kesho.

Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai na Matiko ambaye ni Mbunge wa Tarime Mjini wamekata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana katika kesi ya jinai inayowakabili mahakamani hapo baada ya kupatikana na kosa la kukiuka masharti ya dhamana waliyopewa awali.

Walifutiwa dhamana hiyo Novemba 23 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kufuatia maombi ya upande wa mashtaka kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana kwa kutokufika mahakamani tarehe ambazo kesi yao ilipangwa kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.

Rufaa yao ilipangwa kusikilizwa leo na Jaji Sam Rumanyika kabla ya kusogezwa hadi kesho.

Mbowe na Matiko ambao watarejea mahabusu katika Gereza la Segerea walifikishwa mahakamani hapa mapema leo asubuhi.

Soma zaidi:  Mamia wafurika mahakamani rufaa ya dhamana ya Mbowe

Miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliofika mahakamani hapo ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Bara, John Mnyika, wabunge na madiwani.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi

Soma zaidi: Tafrani yaibuka rufaa ya dhamana ya Mbowe

 



Chanzo: mwananchi.co.tz