Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rufaa kesi ya Gekul yapigwa kalenda

GEKUL11 1 Rufaa kesi ya Gekul yapigwa kalenda

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara, imeahirisha rufaa ya jinai iliyokatwa na Hashim Ally dhidi ya Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul baada ya mjibu rufaa huyo kutopewa wito wa kuitwa mahakamani.

Leo Jumatatu Machi 18,2024 Mahakama hiyo ilipanga kusikiliza rufaa hiyo namba 577/2024, mbele ya Jaji Devotha Kamuzora, lakini kutokana na sababu zilizo nje ya wadaawa (mrufani na mrufaniwa), shauri hilo limeahirishwa hadi Machi 21,2024.

Wakili wa mrufani, Peter Madeleka amesema mahakama haijapeleka hati za wito wala nyaraka za rufaa kwa mjibu rufani.

Katika rufaa hiyo, Ally anapinga maamuzi yaliyofanywa na Mahakama ya Wilaya ya Babati Desemba 27, 2023 ya kuiondoa kesi hiyo mahakamani baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Leo Pauline hukuweza kufika mahakamani ambapo Wakili Ephraim Kisanga anayemwakilisha, ameeleza kuwa siyo mteja wao wala wao(mawakili) hawakuwa wamepokea nyaraka zozote za rufaa na badala yake wamesikia taarifa za rufaa hiyo kupitia vyombo vya habari.

Gekul alidaiwa kumshambulia na kumdhuru Ally Novemba 11, 2023 kinyume cha kifungu cha 41 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live