Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robert ajinyonga kisa hila tu, aacha ujumbe asilaumiwe mtu

Kujinyonga Data Robert ajinyonga kisa hila tu, aacha ujumbe asilaumiwe mtu

Sun, 17 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Robert Lucas Mkazi wa Mtaa wa Ipogoro E Kata ya Ruaha Mkoani Iringa amekutwa amejinyonga chumbani na waya ya umeme kwa kujitundika katika paa la nyumba huku akiacha ujumbe uliosema ameamua kufanya hivyo kwa sababu ya hila tu na asilaumiwe mtu yeyote.

Pracilia Medard ni Mke wa Robert ambapo amesema yeye na mumewe hawakuwa na ugomvi wowote na alikuwa haoneshi kama alikuwa mtu mwenye huzuni bali alikuwa anaona Mume wake yuko sawa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema marehemu aliacha ujumbe unaosomeka “Mimi Robert Lucas nimezaliwa tarehe 29 /9/ 1975 nimeamua kufanya hivi kwasababu ya hila naomba Mke wangu msimsumbue wala Watoto wangu ninaoishi nao na kabla ya mazishi yangu naomba Mdogo wangu Rematus Lucas afike ndio nizikwe “

Mwenyekiti wa Ipogolo E amesema Robert alikuwa na Mtoto ambaye alikuwa anafaya mitihani ya darasa la 7 na Mtot huyo amechukuliwa na Mwalimu wake ili amliwaze huku akisubiri mazishi ya Baba yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live