Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Risiti za EFD zawapeleka Mahakamani

EFDs Risiti za EFD zawapeleka Mahakamani

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

WAFANYABIASHARA 12 wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kuuza bidhaa bila kutoa risti za kieletroniki (EFD) pamoja na kuzuia maofisa kutoka Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kutekeleza majukumu yao.

Watuhumiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama na kusomewa mashtaka yao mbele ya hHakimu David Msalilwa.

Miongoni mwa washtakiwa hao waliofikishwa mahakamani ni pamoja na mmiliki wa Hoteli ya River Mark, Joseph Wabani ambaye alisomewa shtaka lake na kukiri na kuhukumiwa kwenda jela mwezi mmoja ama kulipa faini ya Sh. milioni 1.5.

Kwa upande wake, Hakimu Mkazi wa Wilaya Kahama, Donacian Agustino, aliyesikiliza kesi ya mtuhumiwa Lucas Kishimbe anayemiliki duka la bidhaa za jumla na usafirishaji, alimhukumu mshtakiwa huyo kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini Shilingi milioni tatu baada ya kukiri kosa lake.

Watuhumiwa wengine kesi zao zitaendelea kusikilizwa leo katika mahakama hiyo.

Meneja wa TRA, Warioba Kanire, akizungumza na waandishi wa habari, alisema wameanza kuchukua hatua za kisheria kwa wafanyabiashara wanaokaidi agizo la kutumia EFD katika biashara zao.

Kanire alisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanatoa risiti zenye thamani pungufu ya kiasi cha fedha walichopokea na kuzuia maofisa wa TRA kutekeleza majukumu yao na wengine wakiitwa ofosini kwake wanakataa kufika.

Alisema TRA imekuwa ikitoa elimu kila mara ya ulipaji wa kodi kwa wafanyabiashara waliopo wilayani Kahama, lakini wengi wao wanakaidi kufuata maelekezo hali inayosababisha serikali kukosa mapato yake.

Kanire alisema jumla ya wafanyabiashara 12 wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya kutokuwa na mashine za EFD huku wengine wakitoa risiti zenye upungufu wa fedha wanapouza bidhaa.

Alizitaja baadhi ya kampuni zilizofikishwa mahakamani kuwa ni pamoja na Magnam Resources, Submarine Hotel, Kitapela Investment, Chillers Night Club, Emmanuely Kidenya, Juma Daud Saguda, Cosmas Joachim Mushi, Ushirombo Phamas, bernad Kalamu Lyaka, Rivermak Hotel, Steven Mathias Masunga na Adelina Sylivester Mallya.TR

Chanzo: ippmedia.com