Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ripoti ya Wizi Makongolosi yakabidhiwa TAKUKURU

Zege Mifuko ya saruji ikiwa ni sehemu ya vifaa vya ujenzi

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Agizo la Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Mayeka Mayeka la kumtaka Mkurugenzi kuunda kamati ya kuchunguza wizi wa vifaa vya ujenzi katika kituo cha afya mamlaka ya mji mdogo makongolosi limetekelezeka ndani mwezi mmoja.

Ambapo kamati ya uchunguzi imemkabidhi Taarifa kwa mkuu Mkuu wa Wilaya na yeye ameikabidhi Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) ili kuchunguzi zaidi na wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Akitoa taarifa hiyo kwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mayeka amesema ameridhishwa na utendaji kazi wa kamati iliyohusika kuchunguza madudu yaliyofanyika kituo cha afya makongolosi ambapo amedai kwa wale wote watakao bainika kwenye lolote sheria itachukua mkondo wake.

Aidha Mayeka amepongeza Kamati hiyo iliundwa na Mkurugenzi wa Halmshauri kwa kufanya kazi nzuri na kwa wakati ili haki iweze kutendeka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya ya Chunya Bosco Mwanginde akizungumzia hilo amesema hawezi kuona baadhi ya watumishi wachache wakiendelea kukwamisha miradi ya maendeleo kama ilivyo kwenye kituo cha afya makongolosi.

"Lazima tufanye kazi kwau makini na uadilifu ili kuondoa sitofahamu kwa wale wanaofika kwenye miradi hiyo" alisema Mwanginde. Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la lupa, Masache Kasaka akizungumzia hilo amesema wasimamizi wa miradi kupitia hilo waweze kujifunze kwani na kudai kuwa si mradi huo pekee una changamoto lakini pia kuna baadhi ya miradi tunayotembelea tumekuwa tukikutana na changamoto kadha wa kadha hivyo lazima wasimamizi wabadilike na wafanye kazi kwa weledi.

Ikumbukwe kuwa Novemba 10, 2021 katika kikao Cha kawaida cha baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Chunya alimwagiza Mkurugenzi wa Halmshauri Tamimu Kambona kufuatilia ni kwanini kituo Cha afya makongolosi makongolosi kimekuwa hakikamiliki kwa wakati

Aidha Diwani wa kata ya Bwawani Sailon Mbalawata ambapo kinajengwa kituo cha afya alisema yeye alifika katika kituo hicho ili awashauri lakini hakupewa ushirikiano na kamati hivyo akaamua kukaa pembeni ili kuepuka kuingilia kamati ya ujenzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live