Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ripoti nyingine ya Jeshi la Polisi kuhusu yaliyotokea Kibiti

E3b43d368d2569b678a490a5c6118104 Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi, David Misime

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi limethibitisha kutokuwepo kwa vitendo vya uhalifu katika Wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji zilizopo mkoani Pwani.

Haya yamethibitishwa na Msemaji Mkuu wa Jeshi Polisi nchini, David Misime, ambaye alieleza kuwa wamefanya operesheni maalumu kwenye wilaya hizo zilizolenga kuwabaini wahalifu na wanaofanya mauaji kwenye maeneo hayo.

"kama mtakumbuka, tulishuhudia vitendo vya uhalifu, vilivyotishia hali ya usalama, kama vile, vitendo vya ukabaji na ugaidi kwenye wilaya za kibiti na Rufiji hasa kuanzia mwaka 2014 hadi 2017. Hivyo tumeendesha operesheni hii maalum kuanzia julai 31 hadi Agosti 2 mwka huu ili kuhakikisha maeneo hayo yanakuwa salama"

Kamanda huyo alieleza kuwa zoezi hilo lilifanywa kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na usalama pamoja na wakazi wa maeneno hayo, na kufanikiwa kukamata silaha pamoja na watu waliokisiwa kujihusisha na vitendo hivyo uhalifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live