Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ripoti maalum: Mauaji yatikisa msimu wa Pasaka

Mwl Herieth Ripoti maalum: Mauaji yatikisa msimu wa Pasaka

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matukio ya mauaji yameripotiwa katika baadhi ya mikoa nchini wakati wa sikukuu ya Pasaka licha ya viongozi wa dini kukemea ukatili huo.

Mkoani Mara, mkazi wa kiji cha Keroti, wilayani Tarime, Marwa Menganyi, anadaiwa kuua mtoto wake, Celina Marwa mwenye umri wa miezi minne kwa kumbana pumzi mdomoni na puani kisha kumdumbukiza kwenye jaba lenye maji hadi kufa.

Anadaiwa kutenda ukatili huo kwa lengo la kuchangiwa fedha za rambirambi kutoka kwenye vikundi vyake, ili imsaidie kumaliza madeni yanayomkabili kijini huko.

Akisimulia tukio hilo mama wa marehemu, Bagheni Marwa amedai mumewe alitekeleza ukatili huo baada ya kuwa amekwenda kufua nguo za mtoto ambako alifuatwa na mtoto mwingine kumpatia taarifa hizo.

"Alikuja ananiambia njoo umwone mtoto amezama kwenye jaba na kweli nilipofika nyumbani nilimkuta kwenye jaba kichwa chini miguu juu," amedai mama huyo.

Ameendelea kueleza kuwa baada ya hapo alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa kiji ambaye alitoa taarifa polisi kuwa kuna kifo chenye utata katika eneo lake, akitaka wafike kuchunguza, lakini mume wake alikataa asichunguzwe na kusema waache, azikwe hivyohivyo, hakuna tatizo.

"Akakataa kabisa, mimi ninaona sababu ni madeni ya vikundi maana vilikuwa vinapishana tu kuja kudai fedha zao, hivyo akaamua kufanya ukatili huo, ili achangiwe rambirambi kutoka kwenye vikundi vyake ili imsaidie kumaliza madeni hayo.

"Kila mara alikuwa anadai kutaka kujinyonga, lakini mama yake akamshauri asifanye hivyo, bali atafute njia nyingine ya kupata fedha kulipa alikokuwa akidaiwa," amedai Wagesa Magheni, mama mdogo wa marehemu.

Mama wa mtuhumiwa huyo, Ester Ntono ameeleza kusikitishwa na tukio hilo huku akikana kuhusika katika mipango ya kuuawa mjukuu wake na kutaka watu waache kumsingizia na kumhusisha katika mipango isiyomhusu.

Jirani wa familia hiyo, Ghati Matiku amedai kuwa baada ya kufika eneo la tukio, walibaini mtoto alitumbukia kwenye maji, lakini cha kushangaza hakuwa amekunywa maji hayo, hali iliyozua utata.

Nyangi Kinga, mmoja wa wanavikundi alikokuwa akidaiwa fedha, alidai mchakato wa kumpa fedha rambirambi ulikuwa tayari umekamilika, lakini baada ya kupata taarifa hizo ilibidi wasitishe na pia kuendelea kumdai deni lao la awali.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyabigerna, Muhere Mang'era amesema kuwa baada ya kubaini utata huo, alita polisi ambao walifika na kuanza uchunguzi kwa kuhoji mama, baba, majirani na uongozi wa kiji ili kupata taarifa kamili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Marck Njera amethibitisha kuwa mwili wa marehemu ulipofanyiwa vipimo, ilibainika kifo chake kimesababishwa na kuzibwa mdomo na pua na kukosa pumzi, si maji ya jaba.

Amesema tayari jeshi hilo limemkamata baba wa marehemu ambaye alidaiwa kuhusika na ukatili huo alipoachiwa mtoto huyo nyumbani kwake na kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi. Baada ya kukamilika, hatua nyingine za kisheria zitafuata.

MWANASHERIA AUAWA Mkoani Dar es Salaam, Alex Mazengero, anayedaiwa kuwa ni mwansheria, ameuawa kwa kucharangwa mapanga na watu wasiojulikana alipokwenda kwenye eneo la mteja wake lenye mgogoro.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtoni Mtongani, wilayani Kinondoni, Stanslaus Mnyonge, amesema Mazengero alikuwa mkazi wa mtaa wake kipindi cha nyuma na alikuwa anafuatilia mgogoro huo kwa muda mrefu.

Amesema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa moja usiku katika eneo la Tegeta Skanska ambako mwanasheria huyo alikuwa akikimbilia kujiokoa, lakini hakupata msaada.

Akielezea tukio hilo, mwenyekiti huyo alisema kijana huyo alikwenda kwenye eneo hilo la ardhi kuangalia eneo la mteja wake ndipo wakajitokeza vijana wanne ambao walimkata kwa panga kichwani.

Amesema mwanasheria huyo alianza kukimbia ili kujiokoa, lakini waliendelea kumkimbiza hadi eneo la Skanska, ndipo alianguka chini na walifika wakamkata zaidi hadi umauti ulipomfika.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amethibitisha kuwapo mgogoro wa ardhi na mauaji hayo.

"Ni kweli kuna mtu mmoja ameuawa kwenye mgogoro wa ardhi, hapa nilipo sina taarifa za kina ila tukio kama hilo lipo," amesema Kamanda Muliro.

Mmoja wa madereva daladala, alisema "marehemu alikuwa anavuja damu maeneo ya kichwani na maeneo ya mikononi kwa wingi sana."

Amesema inasikitisha kuona watu walishindwa kumsaidia kutokana na kwamba watahamishiwa kuhusika na mauaji.

MWALIMU, MWANAFUNZI Mkoani Mbeya, watu wasiojulikana wamevamia nyumba moja wilayani Chunya na kuua mwalimu wa shule ya msingi na mwanafunzi wa shule ya sekondari na kujeruhi mtoto kisha kutokomea kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Benjamin Kuzaga ametaja waliouawa kuwa ni Heriety Lupembe (37) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Mbugani na Ivon Tatizo (15) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Isenyela, wilayani humo.

Ametaja mtoto aliyejeruhiwa ni Haris Mtweve (6) ambaye pia ni mwanafunzi katika Shule ya Msingi Ken Gold ya wilayani humo.

Kamanda Kuzaga amesema tukio hilo lilitokea Machi 31, 2024 saa 2:30 usiku wakati watatu hao wakiwa sebuleni nyumbani kwao katika Kiji cha Kiwanja.

Amesema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa wahalifu hao waaliwavamia watatu hao na kuanza kuwashambulia na baada ya kufanya hivyo walifunga milango kwa nje na kuondoka na funguo.

"Chanzo cha tukio hili hakijafahamika, lakini tunaendelea na uchunguzi, majeruhi ambaye ni mtoto Haris Mtweve anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufani ya Kanda Mbeya na afya yake haijaimarika," amesema Kamanda Kuzaga.

Amesema jeshi hilo linaendelea kufanya msako ili kunasa wahusika wa tukio hilo na kuwachukulia hatua za kisheria, akiomba wananchi ambao wana taarifa zozote ambazo zinaweza kusaidia kunasa wahusika wazitoe kwa siri.

Amesenma wahalifu hao wakikamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria kutokana na kOsa hilo la jinai ambalo adhabu yake mahakamani ni kunyongwa hadi kufa kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura 16.

Baadhi ya wananchi wa kiji hicho cha Kiwanja wamesema walishtuka baada ya mwalimu huyo kutofungua duka lake na simu yake kutopatikana huku pia akiwa hajahudhuria kanisani, hali iliyowatia wasiwasi.

Mwenyekiti wa Kiji cha Kiwanja alikokuwa anaishi mwalimu huyo, Gideon Kinyamagoha amesema walifika nyumbani kwa mwalimu huyo na walipoingia ndani kwa kuvunja mlango, walikuta sururu ikiwa na damu na marehemu wawili wakiwa wamelala chini na majeruhi ambaye ni mtoto akiwa kando.

Amesema wametoa taarifa polisi na askari walifika na kufanya uchunguzi wa awali kisha kuchukua mili na kwenda kuihifadhi Hospitali ya Wilaya ya Chunya na majeruhi alikimbizwa Hospitali ya Rufani ya Kanda Mbeya.

Inadaiwa marehemu aliagiza bidhaa za dukani kutoka Mbeya na watu alioagiza baada ya kumkosa nyumbani kwake na hata kwenye simu waliziweka nje, wakiamini alikuwa ametoka na angezikuta baada ya kurejea. Inasemekana kuwa chanzo cha ugomvi huo ni mwanaume kumtuhumu mke wake kuwa ameanzisha mahusiano mengine nje ya ndoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live