Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais TLS atoa ya moyoni mrundikano wa mahabusu

Dkt Tls Dkt. Edward Hosea, Rais TLS

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa chama Cha mawakili Tanganyika TLS Dkt Edward Hosea ametoa mapendekezzo ya maboresho ya kupunguza mrundikano wa Mahabusu na Kesi katika Mahakama za nchini kwa kusema kuwa ni huu ni wakati sahihi wa kutumia adhabu mbadala.

Amesema kuwa hatua stahiki za haraka zinapaswa kuchukuliwa ili kutoa haki kwa wakati kwani kurundikana kwa mahabusu kuna kwamisha shughuli nyingi za Mahakama.

"Hakuna sababu ya kufunga watu kwa makosa madogo, pia Mkuu wa Kituo ana haki ya kutoza faini kama kesi ni ndogo, pia mwenendo wa sheria ya makosa ya jinai, inaelekeza kuwa Mwedesha mashtaka wa serikali anaweza kumtoza faini mtuhumiwa na kuipunguzia kazi Mahakama, haya ndiyo mapendekezo yetu " Amesema Rais huyo.

Nae wakili wa serikali na Kaimu Msajili wa Watoa Huduma za Msaada wa kisheria Ester Msabazi, amesema ni vema vyombo Vya utoaji haki Kutumia adhabu mbadala ikiwemo kifungo Cha nje Ili kukabiliana msongamano wa wafungwa na mahabusu.

Aidha wamesema kuwa maboresho haya katika utoaji haki yanaenda sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya Mahakama ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa majengo ya kisasa Hadi ngazi ya tarafa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live