Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa kigeni 15266, watanzania 45 wakamatwa biashara haramu ya wahamaji

2efb206589014155105f27e9e36705e1 Raia wa kigeni 15266, watanzania 45 wakamatwa biashara haramu ya wahamaji

Sat, 5 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KATIKA kipindi cha Mwezi Januari hadi Novemba 2020; imefanikiwa kukamata jumla ya wahamiaji haramu 15,266 ambao waliingia nchini bila kufuata taratibu za kiuhamiaji, imeeleza Idara ya Uhamiaji nchini.

Aidha jeshi hilo pia limefanikiwa kuwakamata raia wa Tanzania 45 ambao ndio walikuwa vinara wa kuwasafirisha wahamiaji haramu, pamoja na kushikilia vyombo vyao vya usafiri yakiwemo magari (13), Boti (02) na Pikipiki (16) ambazo zilitumika katika usafirishaji wa wahamiaji haramu hao.

Akizungumza leo jijini Dodoma, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk Anna Makakala, Wahamiaji hao wamechukuliwa hatua mbalimbali kwa mujibu wa Sheria ikiwemo kufikishwa mahakamani na baadhi yao kuondoshwa nchini.

"Hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la wahamiaji haramu wanaoingia nchini kwa makundi kupitia njia zisizo rasmi, wakitoka katika Pembe ya Afrika (Ethiopia)...

"...kutokana na taarifa tulizo nazo tumebaini kuwa wahamiaji wanaoingia nchini wanasaidiwa na baadhi ya wananchi wasiokuwa wazalendo kwa nchi yao," alisema Dk Makakala na kuongeza kuwa, "watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria ya Uhamiaji."

Dk Makakala amewataadharisha wote wanaojihusisha katika biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu na magendo ya binadamu kuacha mara moja, kwani adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 20 au faini ya milioni 20 au vyote kwa pamoja na kwamba adhabu hiyo inaenda sambamba na kutaifisha nyumba au vyombo vya usafiri vilivyotumika

Hata hivyo amevishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa ushirikiano walioupata katika kupambana na wahamiaji haramu nchini.

" Navishukuru vyombo vya ulinzi na usalama, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali na Mahakama kwa namna wanavyoshirikiana nasi katika kesi za Kiuhamiaji.

"Pia ninawashukuru wananchi wazalendo ambao wameendelea kutupatia ushirikiano kwa kutoa taarifa kuhusu wahamiaji haramu,"alisema Dk Makakala.

Chanzo: habarileo.co.tz