Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa china asimulia alivyotapeliwa kwa jina la Waziri Mkuu

Hukumu Pc Data Raia wa china asimulia alivyotapeliwa kwa jina la Waziri Mkuu

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu, imewakuta na kesi ya kujibu, mshtakiwa Bahati Malila (50) na mwenzake, Godfrey Mtonyi(30), wanaokabiliwa na mashtaka sita likiwemo la kujipatia Sh22 milioni kwa njia ya udanganyifu.

Washtakiwa hao wanadaiwa kujipatia fedha hizo, baada ya Malila kujitambulisha kwa mfanyabiashara na raia wa china aitwaye Biao Lin Tang, kuwa yeye ni katibu mhutasi wa Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa ilihali si kweli.

Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi Oktoba 19, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate, baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao wa mashahidi 10.

"Mahakama imepitia ushahidi wa mashahidi 10 wa upande wa mashtaka na hivyo kuwakuta na kesi ya kujibu, hivyo washtakiwa wote wanatakiwa kujitetea," amesema hakimu Kabate.

Hakimu Kabate baada ya kueleza hayo aliwatajia njia tatu za kujitetea ambazo ni mshtakiwa anaweza kukaa kimya bila kusema chochote, pili mshtakiwa anaweza kuapa na njia ya tatu mshtakiwa anaweza kuthibitisha.

Mshtakiwa Malila yeye amedai kuwa atatoa ushahidi wake kwa kiapo na atajitetea peke yake na atakuwa na vielelezo.

Kwa upande wake, Mtonyi amedai kuwa watajiteta kwa kiapo na anatarajia kuwa na mashahidi wawili pamoja na vielelelezo.

Washtakiwa baada ya kueleza hayo, Hakimu Kabate aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba Mosi, 2023 ambapo washtakiwa hao wataanza kujitetea.

"Novemba Mosi mwaka huu kesi hii itaendelea ambapo washtakiwa mnatakiwa kuja na mashahidi wenu pamoja na vielelezo vyenu, ili muanze kujitetea, nasema hivi kwa sababu sitaki kusikia mara shahidi wangu sijui kapata tatizo, hapana ..nataka mje na mashahidi wote ili kesi hii iweze kusikilizwa," amesema Hakimu Kabate.

Baada ya kueleza hayo, mshtakiwa Malila amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutumiza masharti ya dhamana wakati Mtonyi akiwa nje kwa dhamana.

Awali, wakili wa Serikali Frank Michael, aliileza mahakaka hiyo kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi iwapo washtakiwa hao wana kesi ya kujibu au laa.

Katika mashtaka yao sita; yapo kughushi nyaraka, kuwasilisha nyaraka za uongo wakionyesha kuwa zimetolewa na waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa pamoja na kujipatia dola za kimarekani 10,000 kwa njia ya udanganyifu ambazo ni sawa na zaidi ya Sh 22milioni, mali Biao Lin Tang.

Miongoni mwa mashahidi waliotoa ushahidi katika kesi hiyo ni Lin Tang, ambaye ni mfanyabiashara na raia wa China.

Lin Tang, katika ushahidi wake aliieleza mahakama jinsi alivyotapeliwa dola za kimarekani 10,000 kutoka kwa Malila, baada ya kujitambulisha kuwa yeye ni katibu mhutasi wa Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa, wakati akijua ni uongo.

Lin Tang ambaye ni rais wa Taasisi Rais wa Taasisi ya Canton HongKong and Macau Fellow Townsmen Association in Tanzania, alidai taasisi yake ilipanga kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa msaada katika Jimbo la Ruangwa ambalo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassimu Majaliwa ndiye mbunge, ambapo walipanga kutoa dola za Marekani 20,000 kwa ajili ya kuwanunulia watoto wenye uhitaji vifaa mbalimbali vya shule ikiwemo madaftari, vitabu, kalamu na sare za shule.

Alidai ili kufanikisha jambo hilo, alimshirkisha rafiki yake aitwaye John Kilasile kisha akamkutanisha na Malila ambaye alijitambulisha kama katibu muhutasi wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

“Nikiwa kama raisi na mwenyekiti wa taasisi Taasisi ya Canton HongKong and Maccaw Fellow Townsmen Association in Tanzania, niliita wanachana wote na msisaidizi wangu na kufanya kikao cha kusaidia watoto hao katika jimbo la Ruangwa” anasema Lin Tang

Anadai baada ya kumaliza kikao kikubwa lilichoshirikisha wanachama wa taasisi hiyo, walikutana kwa mara ya pili na kufanya kikao kidogo katika Hoteli ya Serena iliyopo Dar es Salaam kilichohusisha watu watano, akiwepo yeye, John Kilasile, Bahati Malila , msaidizi wa Jin Tang ambaye ni Guanhui Su Biaolin Tang na mwanamke mmoja ambaye hakumfahamu kwa jina japo alitambulishwa kama rafiki wa Kilasile.

Katika kikao hicho, walimueleza Malila kuwa wana dola za kimarekani 20,000 ambazo zinatakiwa kutolewa katika Jimbo la Ruangwa pamoja na vifaa vya shule ikiwemo sare za shule, madaktari, kalamu kwa ajili ya kusaidia watoto yatima wanaosoma katika Jimbo hilo.

Lin Tang alidai kuwa Bahati alimueleza shahidi huyo kuwa hitaji la kwanza ili kazi hiyo iweze kufanyikiwa alimtaka atoe dola za kimarekani 10,000 kwanza ili apate vyeti vitatu ikiwemo cheti cha shukrani kinachoonesha wanachoenda kufanya ni chema katika Jimbo la Ruangwa.

“Bahati aliniambia, cheti cha kwanza kitakuwa na jina langu, cheti cha pili kitakuwa na jina la msaidizi wangu na cheti cha tatu kitakuwa na jina la taasisi yetu” alidai shahidi huyo.

Hata hivyo, Lin Tang alitoa dola 10,000 na kumpa Malila ili aweze kutengeneza vyeti hivyo.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa Januari 13, 2020 katika eneo la Msasani, Kinondoni mkoani Dar es Salaam, wakiwa na nia ovu walighushi vyeti vitatu wakionyesha ni vyeti vya kuchangia michango kwa ajili ya kutoa misaada elimu kwa watoto wenye uhitaji, vikionyesha vimetolewa Januari 13, 2020 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, wakati wakijua ni uongo.

Katika mashtaka ya kuwasilisha nyaraka zilizoghushiwa, inadaiwa kuwa Januari 14, 2020 washtakiwa wakiwa wanafahamu na kwa nia ovu waliwasilisha nyaraka za uongo kwa Biao Lin Tang ambazo ni vyeti vya utoaji wa michango kwa ajili ya misaada vikionyesha kuwa vimetolewa na Januari 13, 2020 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, wakati wakijua ni oungo.

Katika shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, washtakiwa wanadaiwa, Januari 14, 2020 katika eneo la Msasani, Kinondoni, kwa lengo ovu washtakiwa walijipatia dola za Marekani 10,000 sawa na fedha za Tanzania Sh 22,950,000 kutoka kwa Biao Lin Tang kwa kudai kuwa zinaenda katika jimbo la Ruangwa ambalo linasiamiwa na mbunge Kassim Majaliwa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa ajili ya ununuzi wa vifa vya shule, wakijua kwamba si kweli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live