Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa Ukraine mbaroni kwa kumiliki nyara za Serikali

Hukumu Pc Data Raia wa Ukraine mbaroni kwa kumiliki nyara za Serikali

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

RAIA wa Ukraine, Olga Kryshtopa (35) ameunganishwa na washtakiwa wengine katika kesi ya kumiliki nyara za serikali zenye thamani ya Sh milioni 19.8 na kusomewa mashtaka upya katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. - Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya kukutwa na kobe hai 116 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Josephat Moyo (52), Deogratious Lugeng'a (40), Cosmas Ndomba (39), Hamza Abdallah (52), Kassim Abdallah (35), Nkanamuli Mgaza (52), Stephano Chedego (51) na Mwaluko Ngomole (41). - Akiwasomea mashtaka mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Amiri Msumi, Wakili wa Serikali, Pancrasia Protas alidai katika siku tofauti kati ya Januari, 2022 na Julai 3, 2022 kwenye maeneo tofauti mkoani Dar es Salaam waliongoza na kufadhili genge la uhalifu. - Watu hao wanaokabiliwa na mashtaka matatu wanadaiwa kununua, kusafirisha na kuuza nyara za serikali ambao ni kobe hai 116 wenye thamani ya Sh 18,935,840 bila kibali cha Mkurugenzi wa Maliasili. - Hakimu Msumi alisema dhamana inaendelea kwa washtakiwa wote kasoro mshtakiwa Deogratious Lugeng'a ambaye mdhamini wake mmoja amejitoa na mshtakiwa Olga Kryshtopa ambaye dhamana yake itasikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Rhoda Ngimilanga. Kesi imeahirishwa mpaka Agosti 9 itakapotajwa. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live