Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa Uingereza aliyekutwa na madini ya dhahabu Tanzania afikishwa kortini

89404 Madini+pic Raia wa Uingereza aliyekutwa na madini ya dhahabu Tanzania afikishwa kortini

Fri, 20 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Raia wa Uingereza, Jean Banton (22) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa mashitaka mawili  likiwemo la kusafirisha madini dhahabu yenye thamani ya Sh29 milioni, bila kuwa na leseni.

Akimsomea hati ya mashtaka, leo Ijumaa Desemba 20, 2019 Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 136/2019.

Simon amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba kuwa mshakiwa anadaiwa kutenda makosa yake, Desemba 6, 2019 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam nchini Tanzania.

Amedai katika shtaka la kwanza, Banton anadaiwa kusafirisha madini ya dhahabu yenye uzito wa gramu 300.7, yakiwa na thamani ya Sh29.,06 milioni  bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka husika.

Katika shtaka la pili, siku na eneo hilo, mshtakiwa alikutwa akimiliki madini hayo, ambayo ni mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwa na kibali kutoka mamlaka husika.

Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yake  hakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa Mahakama Kuu ya Tanzania pekee.

Wakili Simon amedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 2, 2020 kwa ajili ya kutajwa na mshitakiwa amerudishwa rumande.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz