Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa Uganda akutwa na mihuri ya TRA

MBARONI.jpeg Raia wa Uganda akutwa na mihuri ya TRA

Tue, 6 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Kagera, linamshikiria raia wa Uganda akidaiwa kumiliki, kutumia mihuri mitatu ya serikali kinyume na sheria za nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bukoba, Kamanda wa Polisi mkoani humo, William Mwampaghale alisema mtuhumiwa amekuwa akitumia mihuri hiyo kugonga kwenye nyaraka mbalimbali

“Alikuwa akigonga hizo nyaraka kuonesha kuwa zimeidhinishwa na na idara husika ya serikali kwa maana ziko tayari kutoka nje kupitia mpaka wa Tanzania na Uganda, eneo la Mtukula,” alisema na kuongeza kuwa wameamua kuficha jina la mtuhumiwa, kwa vile bado wanatafuta wahusika wengine.

Alisema polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, waliandaa mtego na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Septemba mosi saa 11 jioni Kijiji cha Mutukula, Wilaya ya Misenyi na kwamba alikutwa na mihuri hiyo mitatu aliyokuwa anaitumia mipakani.

“Mihuri hiyo ni ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ofisi ya Kilimo, ofisi ya mionzi na katika mahojiano mtuhumiwa amekiri kutumia kugongea kwenye nyaraka bandia, ambazo huzitumia kuvusha magari mbalimbali kwenda nchini Uganda, ” alisema.

Alisema hadi anakamatwa alishafanikiwa kuvusha magari aina ya fuso tisa na semi trailer mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live