Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa China alipa faini Sh300, 000 kukwepa kifungo

Pingu Mkononi Edited Raia wa China alipa faini Sh300, 000 kukwepa kifungo

Wed, 12 Jun 2024 Chanzo: Mwananchi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu raia wa China, Zheng Zhiyuan (47) kulipa faini ya Sh300,000 au kwenda jela miezi 36, baada ya kupatikana na hatia katika mashitaka matatu likiwemo la kuishi nchini bila kuwa na kibali na kuwazuia maofisa wa uhamiaji kufanya kazi zao.

Zhiyuan amehukumiwa kifungo hicho, leo Juni 12, 2024 na Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamula , baada ya kukiri mashitaka yake.

Mbali na adhabu hiyo, Mahakama hiyo imeamuru mshtakiwa huyo kurudishwa nchini kwao, pindi atakapomaliza kutumikia adhabu yake.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amefanikiwa kulipa faini hivyo kukwepa kifungo.

Mshtakiwa huyo ametiwa hatiani baada ya wakili wa Serikali, Grace Nyarata kumsomewa mashitaka yake katika kesi ya jinai namba 15955 ya mwaka 2024.

Mshtakiwa alikiri mashitaka hayo na kuomba apunguziwe adhabu.

"Mshtakiwa umetiwa hatiani kama ulivyoshtakiwa baada ya kukiri mashitaka yako matatu aliyoshtakiwa nayo, hivyo mahakama inakuhukumu kulipa faini ya Sh100,000 kwa kila kosa au kwenda jela miezi 12 kwa kila kosa " amesema Hakimu Lyamuya.

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Hakimu Lyamula alimuuliza mshtakiwa iwapo ana lolote la kusema ili Mahakama iweze kumfikiria.

Mshtakiwa alikaa kimya na baadaye alijibu (kwa lugha ya Kiingereza, ambayo pia ilitumika kumsomea mashitaka yake) kuwa hana wazo.

Chanzo: Mwananchi