Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa Brazil adakwa KIA akiwa na dawa za kulevya

20669 PIC+DAWA TanzaniaWeb

Thu, 4 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Raia wa Brazil Candido De Oliverira (60) amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa na unga unaodhaniwa ni dawa za kulevya wenye uzito wa kilo 6.1.

Naye  Mkazi wa Bombo mkoani Tanga, Yanga Omary Yanga (65) amekamatwa nyumbani kwake akiwa na zaidi ya kilo 1 za dawa za kulevya aina ya heroin alizokuwa ameficha kwenye mifuko ya plastiki.

Akizungumza leo Oktoba 3,2018 Kamishna wa Operesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Luteni Kanali Fredrick Milanzi amesema wamefanikiwa kuwakamata  watuhumiwa hao baada ya kuthibiti kwa mianya waliokuwa wanatumia kupitisha dawa za kulevya ikiwemo katika viwanja vya ndege, mipakani na Pwani ya bahari ya Hindi.

Luteni Kanali Milanzi amesema leo saa 2 asubuhi wamemkamata , Candido De Oliverira katika Uwanja wa ndege wa KIA akiwa na dawa hizo akitokea Sao Paulo nchini  Brazil.

 

Amesema raia ambaye ana  hati ya kusafiria yenye namba FW90620 alisafiri  kwa ndege la Shirika la Fly Dubai DXD akitokea mji wa Sao Paulo.

“Tuliweka  mtego kwa kushirikiana na wenzetu wa uwanja wa ndege wa KIA na tulipomkagua tulimkuta na unga unaodhaniwa dawa za kulevya aina ya Cocaine wenye uzito wa kilo 6.1 ambao tumeupeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili athibitishe,” alisema Luteni Kanali Milanzi.

Pia amesema  Oktoba mosi mwaka huu saa 8 usiku walimkamata Yanga Omary Yanga maeneo ya  Bombo akiwa na Zaidi ya kilo 1 za dawa za kulevya aina ya heroin.

Luteni Kanali Milanzi amesema  walipata taarifa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na mzigo mkubwa wa dawa hizo  na alikuwa anazisambaza sehemu mbalimbali.

Alisema baada ya kupata taarifa hizo walienda nyumbani kwake wakishirikiana na mjumbe wa serikali wa mtaa huo na walifanikiwa kuingia  ndani nyumba yake na kukuta dawa hizo ambazo zilikuwa kwenye chumba kimojawapo zikiwa zimefichwa kwenye mifuko ya plastiki huku pembeni kukiwa bastola ya Kichina.

“Huyu ni mfanyabiashara wa dawa za kulevya anapokuwa na mzigo anajificha anaishi kama mnyama anayeitwa Digidigi, siku hiyo hatukulala tulikesha ili tumkamate na  siku hiyo alileta ujeuri wakati anafungua geti lake tuliweza kumthibiti,”amesema

Amesema wanafanya utaratibu wa kumfikisha mhakamani hivyo aliwaomba watanzania wanaojihusisha na biashara hiyo na washirika wao kuwa Tanzania si sehemu ya salama  kwao kwa kuwa wamejipanga kuwadhibiti na kupambana nao.

Chanzo: mwananchi.co.tz