Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RPC aonya wanaochoma matairi Mwaka Mpya

0844e206dac973ef631f87daea7aa214 RPC aonya wanaochoma matairi Mwaka Mpya

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limewaonya watu hasa vijana wenye tabia ya kuchoma moto matairi ya magari barabarani kusherekea usiku wa mwaka mpya.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu alitoa onyo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana. Alikuwa akizungumzia doria, misako , upekuzi na opereshani uliofanyika hivi karibuni katika wilaya za mkoa huo.

“Kumekuwa na mtindo wa baadhi ya vijana kuchoma matairi ya magari barabarani kama moja ya njia ya kusherekea hususani usiku wa Mwaka Mpya, vitendo hivi viachwe na visifanyike, tutamkamata yeyote atakayefanya hivyo” alionya Kamanda Musilimu.

Alisema Polisi wamejipanga vizuri kukabiliana na wahalifu na wameendesha operesheni kali ya kuwakamata wahalifu, wakiwemo madereva na bodaboda wanaokiuka sheria, kwa kutovaa kofia ngumu na kubeba abiria zaidi ya moja .

Kamanda Musilimu aliwataka wazazi wasiwaache watoto kuzurura hovyo barabarani bila ya uangalizi katika maeneo ya burudani au disco toto. Pia alitaka watoto wasijazane ili kuepusha madhara ya kukanyagana na kukosa hewa.

Alisema imezoeleka wakati wa sikukuu watu wengi huacha nyumba zao na kwenda maeneo ya starehe. Aliwaomba wananchi wahakikishe kuna watu kulinda nyumba zao, kwa kuwa zinapopokaribia sikukuu ikiwemo mwaka mpya, wahalifu hujaribu kujipatia vipato kwa njia zisizo za halali.

Chanzo: habarileo.co.tz