Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RPC aeleze kilichomponza kigogo wa Bavicha

61542 BAVICHA+PIC

Thu, 6 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Polisi mkoani Morogoro limewakamata viongozi watatu wa Baraza vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) wakiwa mji mdogo wa Ifakara wilayani Kilombero wakituhumiwa kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba.

Kati ya waliokamatwa ni Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick Ole Sosopi na wenzake wawili Daniel Ngogo na mwingine hajafahamika.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Juni 6, 2019 amesema watu hao wamekama Ifaraka na wapo njiani kupelekwa kituo kikuu cha polisi mkoa wa Morogoro.

"Watakapofika tutawafanyia mahojiano, walikuwa wakifanya kampeni za nyumba kwa nyumba wakati wakijua ni kinyume na kipindi cha kampeni hakijafika," anesema Mutafungwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz