Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Malima atoa siku 7 walioua albino wakamatwe

RC Malima Atoa Siku 7 Walioua Albino Wakamatwe RC Malima atoa siku 7 walioua albino wakamatwe

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: Eatv

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima ametoa siku saba kwa viongozi  wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo kufanya opereshi na kuwakamata waliohusika na mauaji ya Joseph Mathias mwenye umri  wa miaka 50 mkazi wa Kijiji cha Ngulla Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza ambae ni mlemavu wa ngozi.

Joseph ameuwawa kwa kukatwa panga na watu wasiojulikana kwenye mkono wake wa kulia usiku wa kuamkia leo Novemba 3/2022 akiwa nyumbani kwakwe.

Inaelezwa kuwa watu hao ambao idadi yao bado haijafahamika walivamia nyumba aliyokuwa akiishi Joseph Mathias na familia yake na kisha kutekeleza mauaji hayo

Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu mkoa wa Mwanza Alfred Kapole amesikitishwa na tukio hilo na kuiomba jamiii kuacha kufanya vitendo vya kikatili kwa upande wake Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Mairi Makori amesema hadi Sasa tayari wanawashikilia watu watatu katika tukio hilo.  

Chanzo: Eatv