Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Kagera aahidi kuwachukulia hatua watumishi wala rushwa

Fatma Mwassa.jpeg RC Kagera aahidi kuwachukulia hatua watumishi wala rushwa

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa amewahakikishia Wananchi wa Manispaa ya Bukoba kuchukua hatua kwa watumishi wasio waadilifu wanaoendelea kujihusisha na rushwa na ubadhilifu wa mali za umma.

RC Mwassa alifanya mkutano na wafanyabiashara na Wananchi katika kata ya Bilele viwanja vya soko kuu Manispaa ya Bukoba ambapo alitumia mkutano huo kutoa ufafanuzi juu ya ujenzi wa soko jipya la Manispaa ya Bukoba pamoja na stendi mpya ya kisasa ambapo amewahakikishia Wananchi kuwa kabla ya ujenzi kufanyika tayari Kuna viasharia vingi vya rushwa vimeonekana.

Baadhi ya Wananchi walisimama na kumuuliza Mkuu wa Mkoa ni lini ujenzi wa stendi ya kisasa utaanza baada ya hivi Karibuni ujenzi kusimama katika eneo la Kyakairabwa na huku wengine wakitaka kujua je soko litavunjwa bila taarifa au watawahamisha na kuendelea na ujenzi ???

Mkuu wa Mkoa alisema kuwa serikali ilitoa Sh bilioni 1 kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi wa stendi mpya ,lakini badaaye serikali iliwaingiza Bukoba katika mradi mwingine unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ambao utatekeleza ujenzi wa soko na stendi ya kisasa kwa mwaka 2024/2025.

Alisema kuwa wakati anaapishwa kuja Kagera kama Mkuu wa Mkoa alimkuta mkandarasi anaendelea na maandalizi ya ujenzi wa stendi mpya bila kuwa na mchoro wala ramani ya ujenzi na ndipo akaamua kumbana mkandarasi huyo amueleze anawezaje kuanza kazi ya ujenzi bila mchoro ?! Na mkandarasi alisema ameambiwa asaini hivyo hivyo michoro itamkuta .

Alisema hata hivyo baada ya kumsimamisha mkandarasi huyo mkandarasi alisema kuwa tayari ameombwa asilimia 10 ya kazi yake kutoa kwa baadhi ya watu ambao hakuwataja majina Kama sehemu ya shukrani ya kumpatia kazi ambapo mkandarasi huyo alitoa Sh milioni 50 na bado ajajua ni kwa jinsi gani atapata kurudishiwa fedha zake kwani kazi haufanyiki tena kwa Sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live