Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yawasaka walioua kisha kuondoka na nyeti

Hukumu Pc Data Polisi yawasaka walioua kisha kuondoka na nyeti

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limewahakikishia hali ya ulinzi na usalama Wananchi wa Kijiji cha Mwagig'hi, Kata ya Nkalalo, Wilaya ya Kwimba sambamba na kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya watuhimiwa waliohusika na mauaji ya Masanja Kefa kisha kuondoka na nyeti zake.

Hayo yamebainishwa leo Februari 26 na Afisa Polisi Jamii mkoa wa Mwanza kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhani Sarige akiwa ameambatana na baadhi ya maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wakati akitoa elimu ya Polisi Jamii kwa wakazi wa kijiji hicho.

ACP Sarige amesema Jeshi la Polisi litawasaka wahalifu wote waliohusika na mauaji ya Masanja Kefa (32) Mkazi wa Kijiji cha Mwagig'hi, Kata ya Nkalalo, Wilaya ya Kwimba na kukata sehemu zake za siri na kutoweka nazo kwa kile kinachodaiwa ni imani za kishirikiana.

"Tumewaletea Polisi Kata lengo likiwa ni kuimarisha ulinzi shirikishi lakini mmempokea kwa tukio hili la kikatili sasa si vyema kuendekeza vitendo hivi vya kishirikiana pia tuhakikishe tunashirikiana katika ulinzi shirikishi ili kukomesha vitendo hivi,"amesema afisa huyo wa Polisi Jamii

Mbali na kutoa pole kwa ndugu, jamaa na familia ya Masanja, ACP Sarige amewahakikishia wananchi hao kuwa Jeshi hilo litaendelea kuwa karibu nao na litahakikisha watuhumiwa wote wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha, amewataka wakazi wa eneo hilo kuhakikisha wanatoa taarifa za wahusika wa tukio hilo lilitokea Februari 12 mwaka huu ili kulisaidia Jeshi la Polisi katika upelelezi wake unaoendelea kwa sasa ili kuhakikisha watuhumiwa wote wanatiwa mbaroni na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

"Tunajua watu hawa mnawafahamu na wengine wanaweza kuwa ni ndugu zetu hivyo tusiwafiche wahalifu hawa kwani leo kwake kesho kwako kama kafanya hivyo kwa huyo umemtunza kesho atakufanyia wewe,"amesema

Baadhi ya Wananchi wa Kijiji hicho wamelipongeza jeshi hilo kwa kuendeleza ushirikiano na kuwa karibu nao katika kipindi hiki kigumu na kuahidi kutoa ushirikiano katika kuwapata wahalifu wote waliohusika na tukio hilo na kwenda kuwatolea ushahidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live