Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yawasaka waliojeruhi Wakulima Same

Mkuu Wa Wilaya Same Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni ameagiza Jeshi la Polisi kuwatafuta popote walipo wafugaji wanaodaiwa kuingiza mifugo kwenye mashamba ya watu na kuwajeruhi wakulima watatu wa kijiji cha Kisiwani-Barazani kata ya Kisiwani Wilayani humo.

Ameagiza pia wafugaji wote ambao wameingia kinyemela bila kufuata taratibu za kisheria kuondoka mara moja katika Wilaya hiyo, kabla msako haujaanza na watakao bainika kukaidi sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.

Amesisitiza wakazi wa kijiji hicho ambao wengi wao ni wakulima kuendelea kuwa watulivu wakati vyombo vya Usalama vikiendelea na kazi yake, kuacha kujichukulia sheria mkonini kutaka kulipizia kisasi.

Amewataka viongozi hasa wa vijiji kusimamia sheria kuacha tabia ya kuwapokea wafugaji wageni wanaoingia kinyemela bila kufuata taratibu za kisheria ambao mara nyingi ndio husababisha uvunjifu wa Amani kwa kutoheshimu shughuli nyingine zinazo fanyika ikiwemo kuingiza mifugo kwenye maeneo ya mashamba.

"Wote mnafahamu mfugaji akitaka kutoka eneo moja kwenda sehemu nyingine lazima awe na Barua kutoka uongozi wa serikali ya anapotoka, kisha hiyo Barua aipeleke kwenye kijiji anachotaka kuhamia na viongozi wa kijiji watajadiliana badala ya hapo utaratibu unaonesha kunatakiwa kuitishwe mkutano mkuu wa kijiji Kwa ajili ya wananchi wote kujadili akikunaliwa ndio aruhusiwe na maeneo mengi hamfanyi hivyo mnachokwepa ni nini!?' Alisema Kasilda Mgeni mkuunwa Wilaya ya ya Same.

Kwa upande wao wakulima wa kijiji hicho wamemueleza mkuu huyo wa Wilaya kuwa walilazimika kufikisha malalamiko Yao ofisini kwake kwakua hawapati msaada kutoka Kwa viongozi wao wa vijiji wakiwatuhumu huenda nao wanahusika kuruhusu mifugo kuingiza kwenye maeneo ya mashamba.

Mhe.Mkuu wa wilaya tunavyo fahamu migogoro kama hii ungetakiwa kupata taarifa kutoka Kwa viongozi wao wawasilishe kwako kama ikiwashinda hofu yetu ni kwamba kama wao tukipeleka malalamiko yetu hawatusaidii na kwako taarifa hazikugifii kuna nini hapa, baadhi ya hawa viongozi wa vijiji wanahusika kuchochea". Alisema mmoja wa wakazi wa kijiji cha Kisiwani Barazani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live