Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yawasaka walioharibu mali ugomvi wa familia

HUKUMU Polisi yawasaka walioharibu mali ugomvi wa familia

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linawatafuta watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali katika Kijiji cha Halungu-Mbozi, mkoani Songwe.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa songwe, Theopista Mallya ambapo amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa ardhi unaohusisha familia mbili kati ya watoto wa mke mkubwa na mke mdogo wa marehemu, Focus Makonongo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwakushirikiana na maafisa kilimo Wilaya ya Mbozi linafanya tathimini ili kuweza kujua thamani halisi ya mali iliyoaribiwa pamoja na kemikali iliyotumika kufanya uharibifu huo.

Aidha Jeshi hilo linatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za mtu au watu ambao wamehusika katika tukio hilo ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live