Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yawadaka madereva vichomi 384

Madereva Vichomi Polisi Polisi yawadaka madereva vichomi 384

Wed, 13 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limefanya operesheni mbalimbali za kustukiza za ukaguzi wa mabasi yaendayo mikoani na kukamata mabasi 1918 katika kipindi cha Machi 7 hadi April 10 mwaka huu, huku madereva 384 wakikutwa na makosa hatarishi yaliyopelekea kukamatwa wakiwemo madereva waliokuwa wakiendesha kwa mwendo kasi mkoani hapa.

Akizungumza na madereva wa mabsi hayo katika kijiji cha Mkambarani barabara kuu ya Pwani-Morogoro mkoani hapa, Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu amesema katika operesheni hizo za kustukiza tangu Machi 7 hadi April 10 mwaka wamefanya ukaguzi wa mabasi 1918 na kukamata madereva 384 ambao wamehusika kwa kufanya makosa hatarishi barabara ikiwemo mwendo kasi.

Kamanda Musilimu amesema kuwa hatua hiyo inalenga kuwabaini kisha kuwadhibiti madereva wote wanaoendesha magari kwa mwendo kasi ikiwa sehemu ya kuzuia ajali zinazotokana na uzembe na kukosa umakini kwa kutofuata sheria, michoro na alama za barabara.

“Tumebaini kuwa baadhi ya madereva wanaoanzia safari katika kituo cha mabasi cha Mbezi jijini Dar es Salaam kwenda mikoa ya nyanda za juu kusini, mikoa ya kanda na kanda ya ziwa wamekuwa wakiwahi kufika kituo cha mabasi cha Msamvu tofauti na ratiba yao inavyoonyesha hivyo ni dhahili kuwa wamekuwa wakiendesha vyombo hivyo kwa mwendo kasi usiozingatia micheo, alama na sheria za usalama barabarani.”amesema Kamanda Musilimu.

Kamanda Musilimu ameongeza kwa kusema kuwa lengo la operesheni hizo ni kuwabana madereva wanaokiuka taratibu za sheria zilizowekwa kwa sababu jeshi limebaini mabasi yanayoanzia safari kituo cha Mbezi Dar es Salaam wanapoingia Morogoro baadhi ya madereva wamekuwa wakiendesha kwa mwendo kasi na wanapofika maeneo ya Mikese, Mkambarani na Kingolwira hulazimika kusimama na kuwataka abiria kuchimba dawa wahofia kupigwa faini na askari kwa kufika mapema Msamvu kabla ya muda wao.

Dereva wa kampuni ya mabasi ya Al Saed, Ramadhan Shemdoe alisema operesheni hizo zinasaaidia kupunguza ajali zinazosababishwa na mwendo kasi kwa dereva kushindwa kuzingatia alama za usalama barabarani.

Mmoja wa abiria, Juma Ramadhan alisema ukaguzi huo anaona unazingatia kukumbushwa kwa madereva kuwa na uweledi zaidi katika kazi yao ya udereva na kusaidia kuwa na umakini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live