Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yawadaka 52 walioingia porini kufanya tambiko

33534 Pic+poliasi Tanzania Web Photo

Wed, 26 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Polisi mkoani Mara inawashikilia watu 52 wa jamii ya Watatoga kutoka wilaya za Bunda na Serengeti mkoani humo kwa tuhuma za kuvamia Pori la Akiba la Ikorongo kwa madai ya kufanya tambiko.

Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Desemba 26, 2018 amesema watuhumiwa wakiongozwa na mganga mmoja wa kienyeji ambaye hakumtaja jina walikamatwa jana Jumanne nyakati tofauti katika eneo la Iharara Issenye.

Amesema hawakuwa na kibali na baada ya kuzuiwa walikusanyika na kuanzisha vurugu wakirusha mishale na kumjeruhi askari mmoja wa Kampuni ya Grumeti Game Reserves Ltd.

Hata hivyo, amesema askari huyo alipelekwa zahanati ya kampuni hiyo kwa ajili ya matibabu na anaendelea vizuri.

Amesema askari wanaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine na baada ya kuchambua wahusika watafikishwa katika vyombo vya sheria.



Chanzo: mwananchi.co.tz