Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yautaja 'uhalifu' changamoto kuu Dar

Pingu 1024x769 Polisi yautaja 'uhalifu' changamoto kuu Dar

Mon, 7 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema kuwa hangamoto kubwa inayolikabili jeshi la polisi jijini humu ni vitendo vya uhalifu mabavyo vinachochewa na hali ya jiji kwa la kibiashara zaidi.

Ametoa kauli hiyo wakati akifanya mahojiano na kituo cha habari cha Mwananchi na kungeza kuwa changamoto hiyo inatokana na wingi wa watu walipo jijini humo.

" Tuna changamoto ya Jiji la Dar es Salaam, kama sehemu ya jiji la kibiashara. Changamoto kubwa ilikuwa ni uhalifu wa kuwania mali na kutaka pesa ya moja kwa moja mkononi" Muliro

Ameongeza kusema kuwa Changamoto ni jinsi ya kushughulika na uhalifu wa kijinai. Sheria zimeweka wazi jinsi ya kushughulika na uhalifu wa kijinai, pia zimeweka wazi muda wa kumshikilia mtuhumiwa huyo.

"Kwa mfano X anaibiwa TV yake, ufuatiliaji unafanyika, Y anapatikana ndiyo mtuhumiwa. Kwa mifumo ya kisheria, pamoja na wizi uliofanyika na kuvunja nyumba yako, huyo bado ni mtuhumiwa na dhamana ni haki yake" Amefafanua Muliro

Muliro amesisistiza kuhusu umuhimu wa jamii kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuweza kupunguza matukio yanayoiaha jamii kwenye sintofahamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live